Goma : Askari walio kwenyi mapambano waishi katika hali ngumu alaumu mwanabunge wa taifa Jean Baptiste KASEKWA

Mwanabunge wa taifa Jean Baptiste KASEKWA alaumu hali ngumu ambamo waishi askari jeshi kwenyi mapambano mjini Béni ili kurejesha usalama eneo hilo la Kivu ya kaskazini.

Alinena hayo hii juma nne tarehe 6 aprili wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenyi jumba la UNPC mjini Goma.

 » Ni jambo la kulaumu kutokana na maisha ya askari jeshi wetu kwenyi mapambano ambayo ni magumu na haieleweki .Kwenyi mapambano mjini Béni muda wa miezi kumi na minne, wanajeshi wamepata chini ya dola elfu makumi sita za marekani ambazo kwa mwezi ni dola za marekani elfu nne mia nane kunako mapambano pa Kanyabayonga Eringeti. Kwa kuwa pesa hizo ni ndogo askari jeshi waonekana kuachiliwa wakila kwanga kila leo alaumu mwanabunge Jean Baptiste KASEKWA.

Jean Baptiste KASEKWA aendelea kunena kwamba ni mhimu iundwe kamisheni yenyi mamlaka na lengo kamili la kufwatiliya pesa kuhusu operesheni za askari jeshi na mengine ili ya kuazibu wote wanaopokonya pesa hizo .

Akiongeza kwamba haiwezekani pesa kuhusu marupurupu ya askari jeshi , ama pesa kuhusu ujasusi ziibwe na kuwa dola elfu mbili peke ndizo zitumiwe , alisisitiza kwamba hiyo yaonekana wizi wa pesa katika matumizi.

Mwanabunge Jean Baptiste KASEKWA alihitimisha kwamba kamisheni itakayo wekwa kwenyi bunge la taifa itaendesha uchunguzi ili kutowa mwanga kuhusu pesa zilizotolewa mjini Kinshasa na serkali dhidi ya askari jeshi.

Tufahamishe kwamba wakati wa mkutano aligusia pia nukta kuhusu askari walioondoka jeshini na ambao waachiliwa na serkali, swala kuhusu viongozi wenyi kupokonya nyumba na viwanja vya serkali na mwishowe shule kwa bure kama alivyo ahidi raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI . Akijibu kwa maswala haya yote ,Jean Baptiste KASEKWA anena kuwa yote haonekana kukwama inabidi serkali afanye mapashwa yake dhidi ya raia.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire