Kivu ya kusini : Raia waonekana kuchoka wakingojea aachiliwe huru Prezidenti wa UNC Vital KAMERHE

Katibu makamu wa chama cha kisiasa UNC jimboni Kivu ya kusini Daniel Lwaboshi asema kuaandaa kazi kadhaa katika amani namna ya kutoa malalamiko kwa kuomba aachiliwe huru Prezidenti wa UNC Vital KAMERHE.

Duru zetu toka mjini Bukavu zaeleza kuwa hayo yalifanyika hii juma nne tarehe 6 aprili kunako jumba la UNC mjini Bukavu.

 » Haiwezekane tarehe nane aprili na mwezi mzima kupita bila kufanya chochote kile. Ni kusema kuanzia hii alhamisi tarehe nane aprili chama UNC mjini Bukavu kinaandaa kazi kadhaa katika amani mfano wa misa na ibada mbali mbali ili kumuweka prezidenti wao Vital KAMERHE mikononi mwa Mungu muweza yote anena kiongozi huyu Daniel Lwaboshi.

Akiongeza kwamba kutaandaliwa kongamano Pia, pamoja na mazungumzo kati ya raia, matendo kuhusu upendo yote katika lengo la kutafuta aachiliwe huru Prezidenti wa UNC Vital KAMERHE.

Katibu makamu wa chama UNC Jimbo Kivu ya kusini anena kuwa raia wameonekana kuwa wameanza kuchoka kuona siku zaendelea bila kupata suluhu kwa shida hiyo.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire