Bukavu : Théo NGWABIDJE KASI ashimika shauri ya vijana jimboni Kivu ya kusini

Liwali wa jimbo la Kivu ya kusini Théo NGWABIDJE KASI akikabizi madaraka

Jimbo la Kivu ya kusini lanena kufahamu jukumu la vijana na shida kadhaa zinazowakumba jimboni. Kwa hiyo Jimbo lasema kufanya yote iwezekanayo ili kuchukuwa mbinu za kuunda kazi, kuinua elimu kiufundi ,pamoja na kujitegemea kikazi ili kuinua vijana hawo ambao ni DRC ya kesho watakaoijenga.

Habari toka chumba cha mawasiliano kwenyi ikulu ya liwali wa Kivu ya kusini zanena kwamba hayo yalisemeka wakati wa kushimika shauri la vijana jimboni Kivu ya kusini hii juma mosi tarehe 10 aprili 2021 mjini Bukavu naye liwali wa jimbo Théo NGWABIDJE KASI.

Duru zaendelea kwamba liwali wa jimbo Théo NGWABIDJE KASI ameomba vijana kuwa na bidii, na umoja , upendo, kufurahi kuhusu kazi ambayo imetekelezwa, kuwa marafiki, kuhusiana, kupenda nchi, kuinua urafikiri , kuwa na desturi ya kuunda, kubadili tabia, na hasa kuwa na mwenendo bora, kuwa raia mwenyi kustahili. Hiyo itapelekea vijana kuaminiwa na raisi wa DRC, na serkali ya Jimbo, na mashirika nchini na zile za kimataifa.

Liwali aliomba pia vijana kuepuka kila kundi za wanjanja na wote wenyi nia mbaya wakizani kwamba vijana ndio silaha zao, ambazo watatumia ndani ya vita zisizofaa kisiasa nchini.

Tufahamishe kwamba ni zaidi ya ya miaka kumi uchunguzi haufanyike kwenyi shauri la vijana jimboni Kivu ya kusini.

Kwa hiyo liwali Théo NGWABIDJE KASI aliruhusu uchunguzi huo ufanyike , kwani apigania hasa haki ya akina mama na vijana duru zafahamisha.

Chumba cha waandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire