Liwali wa Jimbo la Kivu ya kaskazini Carly Nzanzu Kasivita ajulisha kwamba askari polisi na jeshi , viongozi wa kisiasa , shirika la raia wamekaa pamoja hii juma tatu tarehe 12 aprili ili kutafuta suluhu kwa shida iliyopelekeya kifo na majeraha kando ya mji wa Goma na wilayani Nyiragongo. Akihakikishia raia kwamba hali itaendelea kuwa tulivu na kuwa atasaini barua anayo kataza maandamano kwa maana ndimo maadui wa usalama wapitia ili kufanya machafuko.
Alinena hayo mbele ya wandishi habari baada ya kikao cha haraka kilicho fanyika ambamo walishiriki viongozi wa jeshi , wa polisi , wa shirika la raia na hata wenyi kuwakilisha makabila.
Liwali wa Jimbo afahamisha kwamba yote yameanza kutokana na mwendesha pikipiki moja wa huko Kibumba aliyeuliwa hii juma pili kupitia hali ya heka heka eneo hilo . Pamoja na hayo kuchomwa kwa moto nyumba na raia wenyi nia mbaya. Hiyo imepelekea askari polisi kufanya kazi yao.
» Askari polisi wanapatikana nafasi hizo ili kurudisha usalama na kufahamu matokeo kwani inabidi kufanya mzunguko hata kunako vituo vya afya ili kupata mwanga zaidi »‘ anena liwali na kuongeza : » tunaamini kwamba viongozi kadhaa wametumwa e neo hilo yaani viongozi wa kisiasa, shirika la raia, askari jeshi na polisi watatumika bega kwa bega na kuzima moto. »
Akifahamisha pia tayari amekutana na jamaa la mhanga moja aliye fariki dunia na walikubaliana kuwa mazishi yafanyike pa Kibumba.
Liwali aendelea kuomba raia wabaki kimya na hata vijana akisema kusaini barua ili kukataza maandamano kwa muda ambayo ni chanzo cha vurugu jimboni.
Tukumbushe kuwa maandano iliyo andaliwa na wana harakati wa kiraia yalizusha hali ya heka heka wilayani Nyiragongo na kando ya mji wa Goma ikizaniwa kuwa ni vuta ni kuvute kati ya makabila za huko jambo lilitopiliwa mbali na viongozi walishiriki mkutanoni.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.