Prezidenti wa Muungano wa makabila yaani barza intercommunautaire Alexis BAUMA aalika raia mjini Goma kuwa watulivu kwa kuwa suluhu itapatikana kuhusu hali ya heka heka wilayani Nyiragongo na kando ya Goma.
Alinena hayo hii juma tatu baada ya mkutano na liwali wa Jimbo pamoja na viongozi wengine wa kijeshi, wa polisi , wa shirika la raia na hata wabunge ambamo walikuwa wakitafuta mbinu ili kukomesha hali iliyozuka jimboni Kivu ya kaskazini.
« Ujumbe ni kwamba raia wabaki kimya hali ni kwamba ni vuta ni kuvute ambayo bado kueleweka ila ni watoto wetu ndio wahanga wa vitendo hivyo. Tutajaribu kukomesha shida hiyo . Tutaenda uwanjani ili kutuliza raia wote kwa jumla » anena kiongozi huyu.
Alexis Bauma aomba yeyote aliye jiingiza katika machafuko hayo kuondoka maana inabidi suluhu la kudumu siku za usoni.
Akiongeza kwamba chanzo kanuni cha vurugu hiyo hakijajulikana inabidi uchunguzi kwa makini
Upande wake Mambo Kawaya prezidenti wa shirika la raia wilayani Nyiragongo atupilia mbali swala kuhusu vuta ni kuvute kati ya makabila huko Nyiragongo akialika raia kuwa tulivu wakingojea suluhu toka vyombo vya usalama.
« Tunatoka pokelewa naye liwali wa Jimbo , nazani swala halihusu makabila ni vijana wapotevu wenyi kuzania kuwa ndani ya kundi ambao walionyesha hasira dhidi ya Monusco , wakitumia silaha na kusababisha vifo vya watu wawili . Hayo yalipelekea hasira kwa vijana wengine ambao walianza vuta ni kuvute na wenzao « aeleza kiongozi huyu.
Mambo Kawaya aomba pia raia waendelee kubaki kimya kwa kuwa miili ya wahanga iliweza pelekwa kwenyi chumba cha wafu ili kungojea mazishi.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.