Goma : Muungano wa wapasha habari Kivu ya kaskazini UNPC waomba wandishi habari kuwa na jukumu ndani mwao wakati wa migogoro

Katika barua iliyo somwa naye prezidenti wa Muungano wa wapasha habari UNPC Kivu ya kaskazini MASIKA ZAWADI Rosalie ikisahiniwa pamoja naye KAKULE VAGHENI Jacques katibu tendaji , Muungano wa wandishi habari UNPC Kivu ya kaskazini unashukuru wapasha habari kwa kazi wanazozifanya kila leo katika lengo kuimarisha uhuru wa upashaji habari. Ila watoa tahazari kuhusu habari zenyi kuelekea usalama jimboni Kivu ya kaskazini, mjini Goma na hata wilayani Nyiragongo.

Ilikuwa katika kikao na waandishi habari hii ijumaa tarehe 15 aprili 2021 mjini Goma.

Muungano UNPC Kivu ya kaskazini ukiomba waandishi habari kutochochea kuwa hali ni ya heka heka kuhusu vitendo vingine vya ujeuri vyenyi kuripotiwa ndani ya wilaya zingine jimboni Kivu ya kaskazini.

 » Vyombo vya habari vina haki na mapashwa ya kutangaza habari kwa raia. Muungano UNPC wakumbusha kwamba muda huu inabidi kuchambua habari kwa makini ili kuzuia wale wote wataka mgawanyiko kuzuia hali ya ubaguzi , mawazo mabaya n’a kadhalika.

Kupitia barua hiyo wapasha habari waombwa kujuwa jambo la kueleza maana tamko moja laweza washa moto. Kujuwa jukumu la mpasha habari katika habari ya kutangaza, kuheshimu maisha ya mtu binafsi, kukinga duru inayotowa habari.

Muungano UNPC wakumbusha jukumu la mpasha habari kutangaza habari zenyi kuleta mabadiliko bora kuhusu mwenendo wa wanainchi. Pamoja na hayo kuepuka kutangaza masemi, alama, maandiko na mengine inayo chochea mauaji, rangi, Kabila, Jimbo la kuzaliwa , ubaguzi na kadhalika.

Barua hiyo iliyo somwa naye Masika Zawadi Rosalie yagusiya mambo kadhaa ipatikanayo katika kitabu cha shirika la upashaji habari Syfia Grand Lacs ambamo waomba mpasha habari wa kijamii : kusema bila kuzuru , kuonyesha bila kutonesha, kutangaza bila kuvunja moyo.

Barua hiyo yatowa tahazari kwa yeyote atakae pita kinyume na haya yote asije akapate azabu kulingana na sheria , pamoja na hayo kualika wandishi habari kwa jukumu lao.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire