Goma: Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Olivier TUISHI KAKOTI aomba serkali kutafuta suluhu kuhusu mizozo ya udongo pa Buhene, vision vingt vingt na Turunga mbele ya yote

Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Kakoti mchaguliwa wa wilaya ya Nyiragongo

Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Olivier TUISHI KAKOTI mchaguliwa wilayani Nyiragongo asema kwamba hakuna mizozo ya ukabila huko Nyiragongo. Akisema kwamba ni miaka chungu télé tangu makabila za wanande , bashi , wahutu na kadhalika waishi pamoja eneo hilo la Nyiragongo. Mizozo iliyo zuka siku hizi inatokana na kundi la vijana lililoundwa ili kupinga kuondoshwa kwa raia kwenyi viwanja vyao na serkali.

Mwanabunge Olivier Kakoti alinena hayo hii juma tatu tarehe 21 aprili wanabunge jimboni kivu ya kaskazini walipokutana na ujumbe wa wenzao wa taifa toka mjini Kinshasa ili kutafuta pamoja suluhu kwa shida la usalama mdogo unaokumba wilaya ya Nyiragongo na kando ya mji wa Goma. Hali iliyo pelekea vifo, majeraha na kuchomwa moto kwa nyumba.

« Nazani suluhu itapatikana. Kuna ujumbe wa wanabunge toka mjini Kinshasa. Tangu Jana kamisheni ya uchunguzi iliundwa ambayo itajielekeza maeneo hiyo ili kujuwa kipi cha kufanya. Ingelikuwa heri kutafuta suluhu mizozo yz udongo iliyoko pa Buhene, Turunga na Vision vingt vingt «  anena mwanabunge.

Akihojiwa namna gani vijana waliotaka viondoshwe vikosi vya Monusco DRC kugeuka mizozo ya udongo mwanabunge jimboni huyu anena kuwa tangu mwaka 2018 ndipo kundi la vijana liliundwa kutokana na mizozo ya udongo wilayani Nyiragongo.

« Kwa leo kundi hilo latumiwa na yeyote yule anatoa pesa, kinywaji na kadhalika ili kuleta vurugu na hata kusababisha maafa mjini » anena mcanguliwa wa Nyiragongo.

Mwanabunge Olivier afahamisha kwamba serkali anapotanzua mizozo hiyo iliyozaa kundi la waasi itapelekea suluhu la kudumu.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire