Mwanabunge mcanguliwa wa wilaya ya Nyiragongo aomba bunge kuhusika na hali ya mizozo pa Buhene, Kiisi wilayani Nyiragongo.
Adèle Bazizane ahakikisha kuwa raia waishi huko katika woga na wasiwasi kutokana na maandamano ya amani ya amani iliyo geuka mizozo kati ya makabila na kusababisha vifo vya watu yapata kumi na saba, kuchomwa kwa nyumba na maafa mengine mengi.
Adèle Bazizane ashukuru wanasiasa wenzake waliojihusisha na jambo lisilo la kwao.
Mwanabunge huyu asisitiza kwamba vuta ni kuvute kati ya vijana wamoja wahuni yapelekea watu kutoaminiana pa Nyiragongo na kando yake.
Fununu zanena pia watu kuyahama maskani yao kuenda mjini Goma.
Mwanabunge Adèle Bazizane alaumu vikali hali hiyo . Ndio maana aomba bunge kuunda kamisheni itakayo shuka mahali pa mizozo ili kuelewa chanzo cha vuta ni kuvute kati ya raia walioishi katika amani hapo awali.
Huyu aomba pia vyombo vya usalama kujihusisha ili kugunduwa waruga waruga ili wapewe azabu na wasirudilie. Akiongeza kwamba utakuwa mfano kwa wengine wenyi kutafuta kuacha moto.
Wabunge waomba liwali wa jimbo kuhudumia wahanga wa machafuko hayo na kwamba mjadala kijamii ianzishwe kati ya makabila.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.