Goma : Guy KIBIRA ashukuru wanabunge wa taifa kwa ujumbe wa amani ambao atapeleka kwa raia

Guy Kibira prezidenti wa shauri la vijana kivu ya kaskazini

Akipokelewa na ujumbe wa wanabunge wa taifa toka mjini Kinshasa, prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini Guy KIBIRA anena kwamba alifasiria wachaguliwa gisi mambo yalipitika huko Buhene, Turunga, Kiisi, Majengo na kadhalika.

Guy KIBIRA afasiria kwamba mizozo ilioko eneo hizo siyo ya makabila ila yahusu udongo.

Huyu asema kuomba ngazi zote za serkali kujihusisha ili kuwe na uhusiano kijamii. Aliomba mbele ya wanabunge uchunguzi ufanyike ili kugunduwa wahusika na kuwaweka kwenyi vyombo vya sheria ili wahanga wapate kusadiki.

Kwa kuwa yote yatokana na hali ya huko Béni ambako raia wauliwa kiholela Guy KIBIRA aomba wabunge kufikisha malalamiko kwenyi raisi wa DRC, kwa bunge ili kutafuta suluhu ya kudumu.

Na kuomba pia kuwe na mabadiliko kuhusu mambo ya udongo, kujuwa mwanainchi anastahili hekta ngapi ili kila mtu apate sehemu.

Akishukuru kuhusu mashauri aliyo tolewa na wabunge prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini aomba raia jimboni humo yaani Nyiragongo, Goma, na hasa vijana kukubali kuishi pamoja.

Akiwaomba kutokubali kila anaye nia ya kuwatumikisha kwa njia mbaya, alisisitiza kuishi pamoja ili ya ujenzi wa nchi.

Ujumbe wa wanabunge pamoja na wakilishi wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini

Mwishowe alishukuru ujio wa bunge toka mjini Kinshasa, akiamini kwamba shida za raia Zitajibiliwa ipasavyo kupitia wabunge hawo.

Tufahamishe hawo toka mjini Kinshasa wanaendelea na ziara ya kazi . Hii alhamisi tarehe 22 aprili watashuka kwenyi eneo kuliko fanyika mizozo ili ya uchunguzi.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire