Goma: Kazi za chanjo dhidi ya Corona ni mwanzoni mwa mwezi mei 2021( Nzanzu Syalita)

Kazi ya chanjo dhidi ya Corona zitaanzishwa hii tarehe mosi mei 2021 jimboni Kivu ya kaskazini.

Ndivyo afahamisha waziri wa afya jimboni Kivu ya kaskazini Syalita Nzanzu wakati wa mkutano na wandishi habari hii ijumaa tarehe 21 aprili 2021.

Kwake waziri, chanjo hiyo ni kiasi ya elfu makumi sita yaani 60 mille doses ambayo tayari yamefikishwa mjini Goma. Ila ni elfu mia moja mia tisa yaani 190 mille doses ndio yahitajika kwa jimboni Kivu ya kaskazini.

Chanjo hiyo aina Astrazeneca itatolewa kwa mtu kwa hiari yake na waganga wenyi ujuzi katika vituo kadhaa vya afya

Wanaohusika kupokea dawa hiyo ni watu wenyi umri hamsini na tano na zaidi. Watatolewa pia chanjo hiyo waganga jimboni na wengineo.

Kwa liwali wa jimbo Carly Nzanzu Kasivita kuanzisha operesheni tarehe mosi mei kutaruhusu dawa kufika eneo zingine ambako itatumwa.

Akiomba vyombo vya habari kujihusisha ili watu waje wengi kwenyi chanjo , hii ni namna moja wapo ya kuipiganisha magonjwa.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire