Goma : Kazi za chanjo dhidi ya Corona zitaanzishwa mwezi mei hapa karibuni

Wizara ya afya jimboni Kivu ya kaskazini yanena kuwa kazi za chanjo dhidi ya Corona zitaanzishwa tarehe mosi mei mwaka huu jimboni Kivu ya kaskazini.

Ndivyo anena waziri ahusikae na afya jimboni Kivu ya kaskazini Nzanzu Syalita mbele ya wandishi habari hii alhamisi tarehe 22 aprili 2021 mjini Goma.

Waziri aeleza kwamba ni elfu makumi sita kiasi ya dawa( 60 mille doses) zitatolewa kwa watu wenyi umri wa miaka hamsini na tano na kuendelea kwa hiari ya kila mtu.

Waganga pia watatolewa chanjo na wengineo watakao chaguliwa na watalaam wa afya.Ila ni mia moja tisini elfu ya dawa za chanjo ( 190 mille doses) ndio yahitajika jimboni Kivu ya kaskazini .

Kwake liwali wa Jimbo kuanzisha kazi ya chanjo tarehe mosi mei kutaruhusu dawa kufika eneo zingine ambako zitatumwa. Akiomba vyombo vya habari kujihusisha ili watu waje wengi kwenyi chanjo maana ni namna moja wapo ya kuipiganisha magonjwa.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire