Goma : Carly Nzanzu Kasivita achukuwa hatua akipinga kupokonywa kwa uwanja wa kandanda SOTRAKI

Liwali wa jimbo Carly Nzanzu Kasivita akisindikizwa na wanabunge na viongozi wengineo

Liwali wa jimbo la kivu ya kaskazini Carly Nzanzu Kasivita amechukuwa hii juma nne tarehe 27 aprili hatua ya kujihusisha kinaganaga ndani ya vuta ni kuvute kati ya vijana wa kata Kyeshero na meja Kizito.

Huyu akishutumiwa kupokonya uwanja wa kandanda SOTRAKI jambo lililo pelekea hasira ya vijana kupanda hadi kuweka vizuizi barabarani.

Alipowasili kwenyi nafasi ya heka heka ,liwali wa jimbo alinena kutongojea uamzi wa korti kuu na kukataza haraka kazi za ujenzi eneo hilo.

Akisindikizwa na wanabunge wa jimbo na moja wa taifa Hubert Furuguta alipanza sauti kuhusu wevi ndani ya Jimbo wenyi kuuzisha kimagendo viwanja vya serkali.

Akiahidia raia wa Kyeshero kwamba atajihusisha kisheria ili meja Kizito ahukumiwe na apate kifungo.

Mwishowe aliomba vijana kuondowa mawe barabarani na kutochoma gurudumu , kwani vyombo vya kazi vitapelekwa kwenyi uwanja ili kurudisha sura yake ya awali .

Vijana walisema kufurahishwa na hatua yake liwali wakimusindikiza hadi alipoondoka nafasi hiyo.

Tufahamishe kwamba ni raia wenyi hasira kubwa ndio walishuka barabarani ili kupinga kupokonya kwa uwanja wao wa kandanda.

Juvénal Murhula

1 Comment

Poster un Commentaire