Goma : Mwanabunge Safari Nganizi pamoja na wachaguliwa wake wangojea usalama jimboni Kivu ya kaskazini

Mwanabunge Safari Nganizi mcanguliwa wa wilaya ya Masisi

Akiwa ziarani jimboni Kivu ya kaskazini mwanabunge Safari Nganizi anena kuja humu jimboni ili kukutana na wachaguliwa kuhusu yale wangojea kwa serkali nyipya . Ijapo wapatikana kwenyi kikao bungeni, yeye alipata fursa ya kuja kwani hakuweza fika wakati wa likizo.

Amenena hayo kwenyi uwanja wa ndege mbele ya wandishi habari hii tarehe 29 aprili 2021 mjini Goma.

« Nimekuja jimboni ili kukutana na wachaguliwa. Mwafahamu kwamba tayari serkali nyipya yake Sama Lukonde imetajwa. Kivu ya kaskazini imekumbwa miaka mingi na usalama mdogo Béni, Masisi na Rutshuru. Ingawa mji wa Goma una barabara inje ya mji ni hatari. Tutazungumza na raia kuhusu usalama mashariki mwa DRC hususan jimboni Kivu ya kaskazini ambayo serkali yabidi kutekeleza. » Anena mubunge Safari mcanguliwa wa Masisi.

Akiunga serkali nyipya mkono, aliomba pia wachaguliwa wake kufanya hivyo , wakiunga mkono hata maoni ya Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI, ambaye amejitahidi kuhusu usalama mashariki mwa DRC.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire