Goma : Saasita anena kwamba kujiunga na FCC, CASH hayawezi kwamisha kazi zao kama wanabunge

Wanabunge jimboni Kivu ya kaskazini wakitoka mjini Kinshasa

Mwanabunge Saasita jimboni Kivu ya kaskazini anena kuwa waziri mkuu aliahidi kuhusika na usalama mdogo mashariki mwa DRC hususan jimboni Kivu ya kaskazini wakati wa kushimikwa kwake. Na kwamba atafanya iwezakanayo ili ucaguzi ufanyike mwaka 2023 . Akiongeza kwamba waliweza kutana wana seneti kuhusu shida inayokumba Jimbo la kivu ya kaskazini. Na kwamba kazi zao kama wanabunge zaendelea ijapo kujiunga na FCC pamoja na CASH.

Mwanabunge Saasita anena hayo akiongoza ujumbe wa wanabunge wa jimbo la Kivu ya kaskazini wakitoka ziarani mjini Kinshasa. Ilikuwa hii alhamisi tarehe 29 aprili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma.

« Waziri mkuu alinena wakati aliweza shimikwa kwamba atajihusisha na sekta kadhaa akigusia usalama mdogo unaokumba mji wa Goma, Buhene, Béni, Ituri , Kivu ya kusini na kadhalika. Aliahidi pia kwamba atafanya iwezekanayo ili kutekeleza uchaguzi mwaka 2023″ asema mwanabunge Saasita.

Kuhusu kujiunga na FCC , CASH , huyu alisema kwamba kujiunga na FCC CASH haiwezi kamwe kukamwisha kazi zao kama wanabunge yaani kuunda sheria pamoja na kucunguza kazi za serkali.

Mwanabunge huyu anena kuwa wamekutana na viongozi kadhaa miongoni mwao wana seneti ili kuzungumzia hali inayokumba Jimbo la kivu ya kaskazini.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire