Goma: Adrien SIYASEMBA aomba raia kuunga mkono Raisi wa DRC kwa ppkubadili viongozi wa kiraia na wale wa kijeshi Kivu ya kaskazini na Ituri

Mwanabunge Adrien SIYASEMBA kunako uwanja wa ndege mjini Goma.

Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Adrien SIYASEMBA asema kuwa amejibu kwa mwaliko wake Raisi kuhusu kuundwa kwa serkali nyipya . Akifurahishwa na hatua iliyochukuliwa naye Raisi kwa kubadili viongozi wa kiraia na wale wa kijeshi Kivu ya kaskazini na Ituri. Kwake ni matakwa ya viongozi wa Jimbo la kivu ya kaskazini kuhusu usalama mdogo unaokumba Jimbo hilo myaka chungu tele.

Amenena hayo kwenyi uwanja wa ndege akitokea mjini Kinshasa hii juma nne tarehe 4 mei 2021 mbele ya wandishi habari.

« Nimetoka mjini Kinshasa ambako tulialikwa kushiriki kuhusu kushimikwa kwa serkali nyipya » anena mubunge huyu.

Akihojiwa kuhusu kubadili viongozi wa kiraia na wale wa kijeshi Kivu ya kaskazini, Adrien SIYASEMBA anena kuwa hiyo ni matakwa ya viongozi wa Jimbo la kivu ya kaskazini tangu awali.

Akinena kuwa mawaziri, wana seneti , wanabunge wa taifa na wengineo walifanya utetezi kunako ngazi za juu ili serkali nyipya itekeleze usalama mashariki mwa DRC hususan jimboni Kivu ya kaskazini.

Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Adrien SIYASEMBA anena kuwa serkali iliyotangulia haikufaulu ndio maana aomba raia kuunga mkono hatua yake Raisi ili amani itande Kivu ya kaskazini.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire