
Tarehe 3 mei kila mwaka, ulimwengu mzima yasherekea siku kuu ulimwenguni ya uhuru wa upashaji habari.
Mjini Goma sherehe iliandaliwa na Muungano wa wapasha habari UNPC kwa ushurikiano na Shirika la Redio na Televisbeni Kivu ya kaskazini CORACON maarufu.
Wandishi habari walikusanyika wengi hii juma tatu katika mada : Habari ni kwa wote
Kutokana naye Bwana Valérie MUKOSASENGE ahusikae na mwenendo wa wapasha habari kwenyi UNPC, ilikuwa fursa ya kuchunguza kazi wanazozifanya wandishi habari kila leo . Nini imeendeka na nini haikuendeka na nini inatarajiwa kufanyika munamo siku za usoni ili kuboresha kazi.
Kiongozi wa Muungano wa kutetea haki za wandishi habari JED Tuver WUNDI alifasiria gisi apashwa jikinga mwandishi habari wakati wa maandamano. Akiomba mbele ya yote mpasha habari kujuwa hali gani ambamo maandamano yafanyika.
Akinena kwamba ingawa maandamano yanaweza pelekea kutupwa kwa mishale inaomba mwandishi habari asiende peke yake.
Pia atafute mahali pa kujificha ambako ni raisi kwa kunyatuka.
Tuver WUNDI aomba wapasha habari kujitambulisha mbele ya yote kwa walinzi wa usalama na kwa waandamanaji.
Wakati huo waandishi habari walitoa shida kadhaa wanazozipata ndani ya kazi wakitoa mfano wa shida zilizowakumba katika migogoro pa Buhene, wengi wakihatarisha maisha.
Naye mwakilishi wa shirika CORACON alishukuru wandishi habari kujibu kwa mwaliko na kuahidi kuendelea kusindikiza vyombo vya habari katika lengo la kuboresha kazi zao.
Juvénal Murhula
,
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.