Kama ilivyo tangazwa kwenyi Televisheni ya taifa RTNC hii juma nne jioni Jenerali Luboya Nkashama ndiye amechukuwa uongozi wa jimbo la Kivu ya kaskazini, makamu akiwa Benjamin Alonga Boni ambaye ni kamisa wa polisi.
Mabadiliko hayo yaambatana na katiba ya Jamhuri ya kidemocrasia ya Kongo yenyi kuruhusu uongozi wa jeshi muda wa siku thelasini na kwamba mhula unaweza endelea ingawa haijafikia lengo.
Upande wa Ituri ni Jenerali Constant Ndima ndiye liwali akisaidiwa naye makamu Ekula Lupopo . Hiyo uongozi wa jeshi ni katika lengo la kukomesha usalama mdogo unaosababishwa na kundi zenyi kumiliki silaha katika majimbo hayo mawili Kivu ya kaskazini na Ituri.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.