Bukavu : Watembeza pikipiki wapinga msako wenyi kuandaliwa na widhara ya ucukuzi jimboni

Eneo moja la mji wa Bukavu.

Waendesha pikipiki mjini Bukavu wapinga hii juma tano tarehe 19 mei msako ulioanzishwa na widhara ya ucukuzi jimboni Kivu ya kusini. Katika lengo la kuchunguza vikartasi vya kazi. Hayo yapelekea hali ya heka heka kunako barabara kadhaa za mji wa Bukavu.

Tangu nafasi ya uhuru kupitia Feu rouge hadi Nyawera na kwenyi eneo zingine za mji , pikipiki zatembea kwa mwendo wa kasi. Zikipiga kelele na kuasha taa ili kuonyesha huzuni.

Habari toka mwenzetu Loni YOEL mjini Bukavu , ni kwamba nafasi zingine watembeza pikipiki waondowa vizuizi kwa hasira na kushambuliya wahusika na uchunguzi wa vikartasi.

Wengine hunena kuwa msako mwengine umekoma hivi sasa.

« Kwa nini misako miwili munamo mwezi moja. Hatujuwe kwa nini msako wa rafla » aeleza mwendesha pikipiki.

Wengine wengi husema:  » Ni juma tatu sasa msako mwengine umehitimishwa. Sijuwe kwa nini kuandaa mwengine. Barabara ni mbovu ijapo kutusumbua kuhusu vikartasi. Msako wafanyika mara moja kwa mwaka . Hatukuweza arifiwa. Tutaondowa misumari barabarani na kuendelea na kazi yetu « mtembeza pikipiki Ghislain Watongoka aeleza kwa hasira.

Kwa ukumbusho , waziri ahusikae na uchukuzi jimboni Kivu ya kusini amejulisha tarehe 18 mei kuanzishwa kwa msako ili kuchunguza vikartasi vya kazi kulingana na bajeti mwaka huu.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire