Goma : Mwanasheria Ekila Likombo akuja kushiriki kwenyi kilio cha mama mzazi wake Bahati Lukwebo baadae atakutana na viongozi wa widhara ya ucukuzi jimboni

Ujumbe unaosindikiza waziri makamu wa uchukuzi nchini DRC Ekila Likombo

Waziri makamu wa ucukuzi nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Kongo mwanasheria Ekila Likombo amejielekeza jimboni Kivu ya kusini ambako atashiriki kwenyi kilio ya mama mzazi wake prezidenti wa seneti nchini DRC Bahati Lukwebo.

Anena hayo hii alhamisi tarehe 20 mei kunako uwanja wa ndege mjini Goma kutoka mji mkuu Kinshasa.

 » Hii ni ziara ya kipekee kwani nakuja mjini Goma, Bukavu hadi Katana Kivu ya kusini ambako nitashiriki kwenyi kilio ya mama mzazi wake prezidenti wa seneti wa DRC Bahati Lukwebo Modeste. Yeye akiwa kiongozi wa Muungano wa chama cha kisiasa AFDC, nami ni moja wa memba wa chama hicho, asema mwana sheria Ekila Likombo.

Huyu aongeza kuwa muda wa ziara yake ,atachukuwa dakika kadhaa ili kukutana na viongozi wa widhara ya uchukuzi jimboni . Namna ya kujuwa jisi hali ilivyo katika sekta ya uchukuzi jimboni Kivu ya kaskazini na kusini.

Akihojiwa maoni yake kuhusu uongozi kijeshi Kivu ya kaskazini na Ituri, waziri makamu wa ucukuzi anena kuwa ni hatua iliyochukuliwa na Raisi wa DRC pamoja na serkali.

« Hatua hii ikichukuliwa naye raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI pamoja na serkali ili kukomesha usalama mdogo unaokumba eneo hizo miaka chungu tele. Nawakumbusha kwamba ijapo uongozi kijeshi, sheria inaamuru kuheshimu haki za msinji za binaadamu , zile zinazohusu uhuru wa binaadamu anena waziri makamu.

Ekila Likombo aomba raia kuunga mkono juhudi zake raisi wa DRC pamoja na serkali ya Kongo ili kukomesha machafuko eneo hizo za DRC.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire