Ujumbe wa wanabunge na mawaziri memba wa Muungano wa chama AFDC na wengineo wapatikana Kivu ya kusini kushiriki kwenyi mazishi ya mama mzazi wake prezidenti wa chama AFDC Bahati Lukwebo

Patrick Munyomo ndani ya ujumbe kwenda kwenyi mazishi Kivu ya kusini.

Ujumbe miongoni mwanabunge Patrick Munyomo mchaguliwa wa Goma ukiongozwa na katibu mkuu wa Muungano wa chama AFDC uliwasili hii hii ijumaa tarehe 21 mei kwenyi uwanja wa ndege pa Goma toka mjini Kinshasa.

Kutokana na mwanabunge Patrick Munyomo, lengo ni kujielekeza jimboni Kivu ya kusini ambako watashiriki kwenyi mazishi ya mama mzazi wake prezidenti wa Muungano wa chama chao AFDC na baaadae kurudi mjini Kinshasa.

 » Tunajielekeza mjini Bukavu kwani kiongozi wa Muungano AFDC amepoteza mama yake mzazi, ambaye ni mama na ni Tate yetu aliyewakilisha chama AFDC. Ni kusema tumekumbwa na kilio . Juma mosi kesho tutashiriki kwenyi mazishi na baadae kurudi mjini Kinshasa, aeleza Patrick Munyomo mchaguliwa wa Goma.

Patrick Munyomo asema kuunga mkono hatua iliyochukuliwa naye Raisi wa DRC Félix Antoine Tehisekedi kuhusu uongozi kijeshi Kivu ya kaskazini na Ituri.

 » Sisi wanabunge wa jimbo la Kivu ya kaskazini tunawasiliana na liwali wa Jimbo mwana jeshi. Kwanza mimi binafsi nilikuwa niki hojiana naye kabla nipande ndege nikimuunga mkono » , anena mwanabunge huyu.

Yeye azani kwamba Kivu ya kaskazini yahitaji usalama mdogo ukomeshwe kinaganaga.

« Raisi wa DRC alichukuwa hatua kuhusu uongozi kijeshi. Tuna matumaini kwamba mara haba suluhu litapatikana na kwamba amani itatanda jimboni Kivu ya kaskazini. » Aongeza mchaguliwa Patrick Munyomo.

Kwa wale wanaomutusi kupitia mtandao , alinena kuwa yeye mchaguliwa, hawezi akajibu watu wa aina hiyo. Hiyo ni ujanja ya watu wenyi nia mbaya, wanaotaka kumchafuwa peke.

« Nimekomaa kati yenu mwafahamu. Kila mtu afanye kazi yake . Watu wanaonitusi hazarani siwezi nikajibu lolote ni ujanja. Ofisi yangu imeanza uchunguzi ili kufwatiliya mambo hayo kisheria » asisitiza Patrick Munyomo.

Kwa raia wenyi kuvunjika moyo kuhusu hali hiyo , mwanabunge awaomba subira , wasijali mambo aina ile. Yeye ataendelea kutekeleza miradi nao bila shaka.

Patrick Munyomo apatikana ndani ya ujumbe wake katibu mkuu wa chama AFDC.

Kwa jina la AFDC katibu mkuu wa Muungano wa chama hicho aongeza kwamba ni katika lengo tu la kilio chake mama mzazi wake mwanzilishi wa chama chao Bahati Lukwebo ndipo waelekea mjini Bukavu.

Akiongeza kuwa ni ujumbe mkubwa toka pande zote za DRC ndio utashirika kwenyi kilio.

Tukumbushe kwamba mazishi ya mwili wa mama mzazi wake mwanzilishi wa Muungano wa chama AFDC yamefanyika hii tarehe 22 mei 2021 pa Katana wilayani Kabare jimboni Kivu ya kusini.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire