Bukavu : Kiongozi wa mtaa wa Ibanda akutana n’a viongozi wa tabaka za chini ili kufahamu shida za raia

Akihojiwa na mpasha habari wa la ronde info kiongozi wa mtaa wa Ibanda Evariste Manegabe Ntaitunda akutanana na viongozi wa ngazi za chini namna ya kujogelea raia wa kata tatu za mtaa huo yaani Nyalukemba, Panzi na Ndendere .

Akizungumza na viongozi wa tabaka za chini wa Nyalukemba :

« Hayo ni kwamba twataka kujogelea raia ili tujuwe shida zao ki usalama, swala kuhusu wahami wa Goma na kadhalika. Kwani ni jukumu letu « aeleza Evariste Manegabe.

Akiongeza kwamba wahami wa Goma wapitia shida kadhaa hasa kupandishwa kwa bei ya chakula . Akiomba wafanya biashara kushusha bei ili kuruhusu wahami hao kununua bila shida.

« Nazali serkali hatahurumia wenyi kufanya vitendo hivyo kwani ni ulozi mtupu » anena kiongozi wa mtaa wa Ibanda.

Kwa jumla ni wahami elfu 4926 ndio wameorozeshwa ndani ya jamaa mbali mbali ambazo zashindwa kulisha watu wao binafsi . Kiongozi huyu agusia pia shida za wahami hao kiafia hasa wenyi kuishi nje ndani ye kempi, akiomba hasa vijana kutokataa kujiorozesha mbele ya viongozi wa kata.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire