Goma : Catherine Furaha aomba wana muziki kuchochea amani ya kudumu

Waziri wa utamaduni nchini DRC Catherine Furaha

Akiwasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma waziri wa utamaduni nchini DRC Catherine Furaha aomba wafanya muziki kwa kila ngazi kuchochea amani katika kazi zao za kila leo.

Amenena hayo mbele ya wandishi habari ajili ya siku kuu ulimwenguni ya muziki inayocherekewa tarehe 21 juni kila mwaka

Mada mwaka huu ni  » Sisi sote kuhusu muziki  » akisisitiza kwamba serkali itajitahidi kutekeleza siasa ili kuhudumiya wana muziki na hata wasanii kwa jumla.

Kuhusu haki ya uundaji kwa wasanii nchini DRC ambayo haiheshimiwe , waziri wa utamaduni Catherine Furaha anena kwamba serkali itajihusisha na hayo yote munamo siku za usoni.

Tukumbushe kwamba sekta ya utamaduni kama ville sekta kadhaa nchini DRC yaonekana kuwa na matatizo chungu télé . Wasani na wengine wapendelevu wa sekta hiyo wafanana kutumika kiholela bila serkali kujiingiza kinaganaga.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire