Akihojiwa na mwandishi wa habari wa la ronde info juma lililopita mratibu wa shirika la wana vijiji Rempart du paysan Bwana GUHANIKA ZIHALIRWA Noé anena kwamba asilimia themanini ya memba wa shirika hilo waliopewa mafunzo waambatana na kilimo ya mimea iliyo sahauliwa, pia asilimia themanini memba wajihusisha na ufundi wa kilimo ili kutowa mazao mengi na kwamba asilimia mia moja wafanya biashara ndogo ndogo kulingana na mikopo toka Muungano wao kwa jina MUSO ikisindikizwa na AVEK.
Mratibu wa shirika Rempart du paysan anena hayo baada ya kukutana na wanamemba wamoja wa shirika wenyi bidii, katika lengo la kuchunguza namna zaendelea kazi wazifanyazo kila leo.
« Baada ya miezi sita , twacunguza pamoja na wana memba wa shirika Rempart du paysan wenyi bidii namna kazi zaendelea. Tulicunguza mambo kadhaa yaani mafunzo tuliyo towa kuhusu mlimo wa chakula , ufundi wa kilimo, kupanda mbegu, shirika la mikopo na kadhalika ». Aeleza GUHANIKA ZIHALIRWA Noé.
Huyu afasiria kuwa mimea kadhaa ya kutoa chakula ilikuwa tayari kutupiliwa mbali tukitaja masunga, mahole, mtama na kadhalika.
« Watu waliacha desturi ya kupanda mimea hiyo ambayo ni chakula. Tulifikiri kuhimiza wanamemba kuhusu kupanda mimea hiyo bila shaka. Pamoja na hayo kuomba watu kutotumia chakula toka mboleo ya kizungu ila watumie inayoambatana na mboleo ya asili. Kwa kuwa kuna mazara kwa kutumia chakula toka mboleo ya kizungu » aendelea kufasiria mwalimu huyu ahusikae na maendeleo vijijini.
Kuhusu matatizo, kiongozi huyu ataja maradhi yenyi kushambuliya mimea mfano mabogi, mahole na kadhalika. Na hiyo yapelekea wana vijiji wamoja kufadhaika.
Alitamka pia kwamba shida ingine yahusu wanamemba wapya wenyi kujiorozesha ndani ya shirika la mikopo wakisha pewa pesa huenda zao.
Yeye pamoja na washiriki mkutano walichukuwa hatua ya kuwaondowa wote wenyi nia ya kuja kuchukuwa pesa pasipo kujiingiza kinaganaga ndani ya kazi.
Tufahamishe kwamba shirika la wana vijiji Rempart du paysan lina sapotiwa na mashirika sawa Initiative d’action pour le Développement Local pamoja na FSHI.
Kuhusu maoni GUHANIKA ZIHALIRWA atamani shirika lao liweze kujitegemea kipesa, likiwa na vitambulisho vya peke na kuunda miradi mbali mbali.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.