Goma : Miili ya wandishi habari Raphaël Kiwongi na Jean Luc Nyembo imezikwa kwenyi shamba la wafu MAKAO.

Wakati wa kusindikiza ya wandishi habari Raphaël Kiwongi pamoja na mwenzake Jean Luc Nyembo kunako makao ya mwisho

Miili ya wandishi habari Raphaël Kihongi wa gazeti Jonction na Jean Luc Nyembo wa Droit à la vérité, imepelekwa hii ijumaa tarehe 16 julai 2021 kwenyi shamba la wafu MAKAO wilayani Nyiragongo.

Wapasha habari wengi, wana memba wa jamaa zote mbili na viongozi wamoja wa jimbo mukiwemo liwali wa jimbo hapo mbeleni Carly Nzanzu KASIVITA walisindikiza miili katika hali ya huzuni.

Ushuhuda kadhaa zilitolewa na wanamemba wa jamaa na wandishi habari walioishi pamoja na wandishi habari hawa ambao ni mfano wa kuiga .Valérie Mukosasenge aliye wakilisha Muungano wa wapasha habari UNPC alitoa ushuhuda kuhusu kazi nzuri walizozifanya wandishi habari hawa.

Akiongeza kwamba si vyepesi kupata watu shujaa kama na hao, ambao walijukana popote pâle nchini DRC . Akiomba kuendelea kuunga mkono kazi walizozifanya ili zisonge mbele. Pamoja na hayo kusogelea jamaa hizi yatima ambazo zahitaji huduma

Mcana kati miili hiyo ilipelekwa kwenyi shamba la wafu MAKAO ambako ibada ndogo ilifanyika na ushuhuda za jamaa mbele ya kuziweka ndani ya udongo.

Kwa jumla watu hawa wawili walionekana kuwa mifano ndani ya jamaa zao kutokana na ushuhuda mbali mbali ya memba wa jamaa. Wakisema kupoteza watu wa maana ambao hawataweza kusahau maishani.

Tufahamishe kwamba Raphael KIHONGI wa gazeti Jonction naye Jean Luc NYEMBO wa gazeti Droit à la vérité walitumika katika uhusiano na viongozi wa DRC kwa jumla na wale wa Jimbo la Kivu ya kaskazini kwa pekee.

Wapasha habari hawa wameacha wajane na yatima

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire