Wana elimu wa Univasti ya kikatoliki la Sapientia na wale wa shirika Pole Institute wamekutana ki elimu na ki utamaduni wakikumbuka, wakimulia na kumuaga Profesa Daktari Ka Mana aliyeaga dunia hapa karibuni.
Sherehe zilifanyika kwenyi Univasti la Sapientia hii tarehe 19 julai 2021 jioni.
Historia ya maisha yake Profesa Ka Mana ki elimu, ujumbe za rambi rambi pamoja na micezo kiutamaduni vilitolewa mbele ya umati na viongozi wa shirika mbili yaani Pôle institue na Univasti la Sapientia
Mwalimu mkuu Ka Mana alihudumia pia vijana maishani mwake ambao walisema kupoteza mtu wa maana maishani mwao.
Mfano ni wake Johnson Ishara prezidenti wa zamani wa bunge la vijana jimboni Kivu ya kaskazini :
« Kiini ya yote iliyotamkwa ndani ya mkutano ni kuhusu historia ya maisha yake Profesa Ka Mana, Ujumbe za huzuni kwa kumulia mwalimu mkuu huyo na kuomba vijana kujiunga pamoja ili kuendelesha kazi zake hata kama ametoweka » anena Johnson Ishara.
Kiongozi huyu wa vijana aongeza kuwa vijana wamefunzwa mengi kupitia mwalimu mkuu Ka Mana, kiraia hasa. Akiongeza kwamba inabidi kuwe na mabadiliko kupitia mafunzo hayo. Watu wapya wenyi kupinga kata kata rushwa wajitokeze, wenyi kupinga uongozi mubaya na kadhalika.
Johnson Ishara alihakikisha kwamba kupitia kazi zake Profesa Ka Mana mabadiliko yameanza onekana kupitia wafwasi wake katika kazi zakupigania haki za binaadam.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.