Liwali makamu wa jimbo la kivu ya kaskazini Rémy EKUKA LPOPO aomba wakandeti katika sekta ya elimu ya kiufundi kufanya kazi za mikono kwa bidii maana yatoa matunda bora kwa nchi . Na kwamba itaruhusu watu hawa kujitegemea. Kwani si kila mtu yule inamubidi kusoma yunivasti na jamii ina haja ya wafundi ili ya maendeleo.
Alinena hayo hii juma tatu tarehe 2 agosti 2021 akianzisha rasmi mtihani wa serkali katika sekta ya elimu ya kiufundi mjini Goma.
Huyu alichukuwa mda mrefu akihimiza wakandeti ambao alifahamisha kuwa waruhusiwa kufanya mtihani katika lugha la kimombo na hata kiswahili. Kwa kuwa kifransa ni lugha itumiwayo ofisini na kiswahili ni moja miongoni mwa kugha za DRC.
Mbele ya hapo Inspekta mkuu jimboni katika sekta ya elimu ya kiufundi Emmanuel Gashamba alieleza kuwa ni elfu 1663 miongoni mwao akina mama mia 506 na wanaume 1157 ndio waruhusiwa kufanya mtihani wa serkali .
Akitaja mikondo chungu tele iliyokubaliwa na serkali yaani userumala, ufundi wa gari, ujenzi, kushona viato, kilimo, kazi ya umeme, kutengeneza mabati, kiganga ya nyama, uvuvi , kupiga picha na kadhalika.
Emmanuel Gashamba afahamisha kwamba vyeti vitakavyo tolewa kwa kadideti hao ni vyenyi samani kama vyeti vingine. N’a kwamba vinakubaliwa nchini na kimataifa.
Baada ya hapo liwali makamu alijielekeza huko Masisi kuhusu lengo lile.
Tukumbushe kwamba waziri ahusikae na sekta ya elimu ya kiufundi nchini Antoinette KIPULU yupo pia ziarani jimboni Kivu ya kusini ajili kuanzisha rasmi mtihani huo wa serkali.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.