Nyiragongo : Nyumba zateketea kwa moto

Nyumba zateketea moto pa Ngangi ya tatu jioni ya tarehe 6 agosti 2021

Nyumba tatu zawaka moto saa kumi na nusu jioni ya ijumaa tarehe 6 agosti 2021 pa Ngangi ya tatu kando na senta Rokcy wilayani Nyiragongo mpakani na mji wa Goma.

Vijana miongoni mwao watoto wenyi umri chini ya miaka kumi na tano walitupa mawe kiasi ambayo ilianza jaribu kuzima moto. Na ndivyo ulipunguza nguvu ya moto.

Jirani wa karibu walijaribu kuokowa vitu kadhaa ijapo vingine viliweza kiteketea. Hadi hapo hakuonekana msaada wa viongozi wa mahali.

Duru za mahali zafahamisha kuwa ni moto toka jiko ndio chanzo ya moto yenyewe na kwamba kwa bahati nzuri hakuna mtu amefariki dunia ya ajali.

Tufahamishe kwamba siku hizi ni eneo hilo limeanza shambuliwa na ajali za moto ambao wasababisha maafa mengi.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire