Kivu ya kaskazini : Wanamugambo waasi wengi tayari wameji salimisha kupitia juhudi za uongozi wa kijeshi

Muungano wa wana harakati wa shirika la raia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo unasema kufurahishwa na juhudi za uongozi kijeshi ingawa kunabaki mengi ya kufanya.

Simon Mukenge moja wa wahimizaji wa Muungano wa wana harakati wa shirika la raia Kivu ya kaskazini

Ulifahamisha hayo hii juma mosi tarehe 14 agosti 2021 wakati wa mkutano na wandishi habari mjini Goma.

Simon MUKENGE moja wa wahimizaji wa Muungano huo ameambia wandishi habari kwamba kuna mafanyikio tangu hatua itekelezwe na viongozi wa nchi.

Akinena kuwa kundi za waasi tayari zimeanza jisalimisha toka wilaya nyingi.

Simon MUKENGE atoa mfano wa wilaya ya Masisi ambako kwapatikana kundi kumi za waasi na kwamba ni wanamugambo elfu 2200 ndio wameji salimisha ndani ya jeshi la taifa.

« Katika wilaya ya Walikale kuna mia ya wanamugambo miongoni mwao viongozi wamekwisha ondoka msituni. » Anena mhimizaji huyo.

« Na kunako wilaya ya Rutshuru , kiongozi moja wa waasi amekwisha jisalimisha na wafwasi wake, ijapo Lubéro ni viongozi wawili ndio wameondoka porini « anena Simon MUKENGE.

Vijana walioshiriki kwenyi usomi wa kikartasi toka Muungano wa wana harakati wa shirika la raia

Huyu aomba viongozi wengine wa waasi kufanya hivyo na kwamba serkali ya DRC iweze wahudumia . Na hiyo itapelekea kundi zingine kuweka silaha chini.

« Tunajua kwamba uongozi kijeshi ndio umesababisha kujisalimisha kwa kundi hizo , na hii ni moja wapo ya maendeleo » anena kiongozi huyo.

Simon MUKENGE asema pia kufurahishwa na juhudi za serkali kwa kuazibu wevi wanao pora mali ya nchi na kuomba juhudi ziendelee.

Na kuhusu uchaguzi wa viongozi wa tume huru ya uchaguzi nchini DRC CENI , kundi zishirikishwe kiraia sawa vile kidini maana viongozi wa kidini waonekana kutoelewana katika kazi hiyo wakitupiana vijembe shoka.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire