Muungano wa prezidenti wa shauri la vijana katika majimbo za DRC unasema kuunga mkono Joella Sambo prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kusini.
Matamshi ni yake Guy KIBIRA mnenaji wa muungano huo pia prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini alhamisi tarehe 19 agosti kwenyi uwanja wa ndege toka mjini Kinshasa. Baada ya kushiriki kwenyi mkutano mkuu wa wakilishi wa shauri la vijana nchini DRC pa Kisantu.
Guy KIBIRA anena kuwa ni vurugu mambo inayo fanyika kwenyi ofisi ya shauri ya usalama jimboni Kivu ya kusini ambako vijana wenyi nia mbaya walipinga uongozi wake Joella Sambo aliekuwa ziarani mjini Kinshasa. Wakiwashawishi vijana wengine.
Nakuja na mwenzetu wa Jimbo la kivu ya kusini ambaye vijana wenyi nia mbaya walifaulu kuleta kasoro alipokuwa ziarani mjini Kinshasa. Mimi kama mnenaji wa Muungano wa shauri la vijana nchini nitajitahidi ili kuboresha mambo katika ofisi ya shauri la vijana jimboni Kivu ya kusini , anena Guy KIBIRA.
Upande wake prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kusini Joella Sambo alisema kushukuru juhudi zake Guy KIBIRA ambaye ameahidi kumuunga mkono. Akiongeza kwamba ametambua mambo katika ziara alioifanya huko Kisantu.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.