Goma : wanachuo wa yunivasti UNIGOM waomba viongozi waanzishe kazi ili kuhitimisha mwaka wa shule

Wanachuo wa yunivasti UNIGOM walionyesha huzuni yao hii ijumaa tarehe 19 agosti kwa kutosoma kutokana na kasoro kati ya kamati ya uongozi ya yunivasti hiyo na watumishi wengine.

Wanachuo hao wakiongozwa na mnenaji wao Bwana Iragire NDAISHIMIYE na makamu wake Mussa ZIHALIRWA walishuka barabarani hadi kwenyi chuo ISC ambako barua ilisomwa mbele ya wandishi habari.

Katika mabango walioipeleka inaandikwa  » Tunacoka tunaomba kurudi shule ili tumalize mwaka. Tunaomba waziri ahusikae na vyuo vikuu na yunivasti kujihusisha ndani ya swala na kadhalika, kama ilivyo andikwa.

Baada ya kusoma kibarua hicho waliendelea kuceza na kuimba nyimbo wakionyesha huzuni kwa kutosoma.

Mnenaji wao Bwana aeleza kuwa wanachuo wengi tayari wamelipa shule ila walimu waonekana wenyi huzuni kwa kutolipwa. Akinena kutohusika na mizozo kati ya kundi hizo husika yaani kamati ya uongozi na walimu .

Akihojiwa naye mnenaji makamu kuhusu nini itafanyika ingawa hakuna suluhu kuhusu shida yao, huyu anena kuwa kuna mambo mengine yatakayo fwata ingawa viongozi wataendelea kubaki kimya.

Tufahamishe kwamba maandamano hayo ya amani yalianza kwenyi jumba lao kunako hospitali kuu ya Goma hadi kwenyi chuo ISC.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire