Goma : Liwali mwanajeshi amerudi toka mjini Kinshasa ambako aliitwa na ngazi za juu

Liwali wa jimbo la kivu ya kaskazini Luteni Jenerali Costant Ndima akitokea mjini Kinshasa

Liwali mwana jeshi wa Jimbo la kivu ya kaskazini Jenerali Luteni Costant NDIMA amerudi mjini Goma toka mji mkuu Kinshasa ambako aliitwa na waziri nchini wa mambo ya ulinzi ili kucunguza namna kazi zaendeshwa na uongozi wa kijeshi katika majimbo za Ituri na Kivu ya kaskazini.

Baadaye aliwapokea pia wabunge wa taifa katika lengo hilo.

Akipokelewa kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma baadaye alijielekeza kweyi ofisi yake ambako aliongeza hapo hapo shauri la usalama jimboni Kivu ya kaskazini.

Akihojiwa maoni yake kuhusu uchunguzi uliofanyika dhidi ya uongozi wa kijeshi . yeye anena kuwa si kwake kutowa kauli yoyote bali kwa viongozi wake.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire