Goma : Hali ya utumwa yaweza punguka ulimwenguni ijapo yatowa faida kwa wahusika( Janvier Murairi)

Janvier Murairi katibu tendaji wa muungano wa shirika la raia husika na haki za binaadam jimboni Kivu ya kaskazini

Tarehe 23 agosti kila mwaka ulimwengu mzima yasherekea siku kuu ya kupiganisha utumwa. Katibu tendaji wa shirika zihusikazo na kupiganisha haki ya binaadam jimboni Kivu ya kaskazini Janvier MURAIRI anena kuwa hali hiyo yaendelea ijapo wengi huzani kuwa yamekoma baada ya ukoloni.

Katibu tendaji wa shirika zihusikazo na kupiganisha hali ya utumwa jimboni anena hayo hii juma tano tarehe 23 agosti mbele ya wandishi habari ajili ya kusherekea siku ulimwenguni ya kupiganisha utumwa.

Janvier Murairi afahamisha kwamba hali hiyo yaonekana kote duniani na hata jimboni Kivu ya kaskazini. Katika kazi mbali mbali, ndani ya migodi , kushurtishwa kingono na kadhalika.

Kiongozi huyu aongeza kuwa ni milioni ya watu ulimwenguni ndio waishi utumwani na wahusika wapata faida kubwa hata kama hali hiyo yatendeka kwa uficho.

Mwishowe katibu tendaji asisitiza kuwa utumwa waweza punguka ulimwenguni. Watu wakifunzwa watatoka ndani ya ujinga, wakiazibu wahusikao na kazi hiyo haramu, wahanga wakisindikizwa kisakolojia na kipesa, kukiwa na ushirika kati ya wahusikao na kupiganisha vitendo hivyo ulimwenguni na kadhalika.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire