Goma: Mwanabunge Jean Paul SEGIYOBE ahadi kufikisha malalamiko ya raia kunako ngazi za juu

Mwanabunge Jean Paul Segiyobe kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma

Akiwasili mjini Goma, Mwanabunge Jean Paul SEGIYOBE anena kuja likizoni ili kuzungumza na wachaguzi wake kuhusu hali waishimo siku hizi jimboni mwake.

Huyu alisisitiza kuhusu usalama mdogo humu jimboni Kivu ya kaskazini. Atajioneya binafsi gisi uongozi wa kijeshi ulioko wa fanya kazi na mawazo ya raia kuhusu uongozi huo ili kufikisha malalamiko kwa ngazi za juu.

Kuhusu kuongeza mhula kwa uongozi wa kijeshi Mwanabunge Jean Paul SEGIYOBE azani kuwa uongozi huo haujafikia lengo , siyo vibaya mhula uongezwe. Inayongojewa na wote ni matokeo mazuri.

Kuhusu migogoro katika kuunda kamisheni ya uchaguzi nchini huyu aomba serkali kuunda kamisheni isio egemea upande wowote.

Na hii inabidi ifanyike mbele ili uchaguzi utakapofika uwe huru na wa haki.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire