Kivu ya kaskazini : Prezidenti wa chama COFEDEC akuja kujioneya hali ya maisha jimboni

Prezidenti wa chama cha kisiasa COFEDEC nchini DRC Bi Kahindo Tshipasa yupo ziarani Kivu ya kaskazini. Ni katika lengo la kupapasa hali ya maisha humu jimboni, namna watumika uongozi wa kijeshi na pia kukutana na raia wa kila aina na hata wafanya siasa. Jambo kuhusu janga la Corona litagusiwa.

Huyu anena hayo alipowasili mjini Goma toka mji mkuu Kinshasa.

Ziara yake yalenga pia kumbukumbu la miaka mbili baada ya kufariki kwake prezidenti wa chama COFEDEC Venant Tshipasa.

« Ni muda pia miaka miwili kiisha kufariki dunia kwake Venant Tshipasa aliye kuwa prezidenti wa chama COFEDEC. Alituacha watoto wenyi kupigania amani Aeleza Bi Kahindo Tshipasa.

Pamoja na hayo asema kuja jioneya gisi zaendeshtwa kazi na viongozi wa kijeshi. Chama COFEDEC chasema kupigania pia usalama jimboni.

Akina mama huyu asisitiza kwamba atakutana na raia kwa jumla , shirika la raia, wafanya siasa na hasa vijana.

N’a kwamba haunge mkono wasemao kwamba vijana ni viongozi wa kesho. yaani vijana wapashwa tumika tangu sasa.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire