
Ni wanamugambo wapiganaji mia nane ndio wamejisalimisha, na silaha za vita yapata mia nne ndizo zimepokonywa na jeshi la serkali FARDC muda huu wa uongozi wa kijeshi jimboni Kivu ya kaskazini.
Ndivyo anena Kanali Ndjike Kahiko ambaye ni mnenaji wa eneo na thelasini na nne la kijeshi mbele ya waandishi habari mjini Goma.
Huyu alikuwa akitowa mwanga kuhusu kazi za askari tangu mwanzo wa uongozi wa kijeshi hadi sasa humu jimboni Kivu ya kaskazini. Akiomba wandishi habari kusindikiza harakati hizo .
« Mimi nafurahi na kazi zinazoendeshwa na uongozi , nawaomba nyinyi wandishi habari kutumika mkono mkononi na jeshi la taifa ili kutekeleza amani mashariki mwa DRC. Najua nyinyi munazo nguvu za kupasha habari . Inabidi kutowa habari za ujenzi na kuepuka habari zenyi kufazaisha askari jeshi wenu « anena Kanali Ndjike mbele ya waandishi habari.
Kiongozi huyu wa kijeshi anena kuwa ni muda wa uhamasishaji dhidi raia wa kila tabaka. Ataja mfano wa viongozi wa kijeshi tayari wamehamasishwa , na kwamba ni fursa kwa wandishi habari wenyi uwezo wa kusambaza habari.
Wandishi habari walikubali kuunga mkono kazi za uongozi wa kijeshi, wakiomba washirikishwe ndani na kupewa habari haraka ili kutangaza habari iliyo ya kweli.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.