Kivu ya kusini : Ujumbe wa wabunge husika na uchunguzi wa uchimbaji madini pa Mwenga warudi mjini Kinshasa

Didier Okito LUTUNDULA mcaguliwa wa mji wa Bukavu.

Ujumbe wa wabunge wa Jimbo la kivu ya kusini ukiongozwa naye mwanabunge Jean Claude KIBALA umerudi mjini Kinshasa toka wilayani Mwenga. Ukinena kuwa madini yanachimbwa kinyume na sheria eneo hilo ambako ulijielekeza ili kufanya uchunguzi.

Mwanabunge Didier Okito LUTUNDULA mcaguliwa mjini Bukavu:

« Ni kutokana na barua tulioandikia bunge la taifa kuhusu uchimbaji madini kinyume na sheria na kampuni ya Uchaina. Yalipelekea waziri wa taifa ahusikae na madini kututuma ili kujionea jisi hali ilivyo » anena Didier Okito LUTUNDULA mcaguliwa mjini Bukavu.

Katika mazungumzo na wandishi habari mjini Goma, mcaguliwa huyu wa Bukavu afahamisha kuwa kampuni ya Uchaina yachimba madini pa Mwenga pasipo kuheshimu makubaliano na serkali kuhusu huduma kwa wakaazi waishio pa Mwenga maeneo ya uchimbaji madini.

Mwanabunge Didier Okito asema kupeleka ripoti kwa viongozi husika mjini Kinshasa ili kutafuta suluhu kwa shida hiyo.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire