Goma: Mtoto mcanga ameogotwa akitupwa kwenyi kata Bujovu

Mtoto mcanga aliyetupwa kunako kata Bujovu

Mtoto mcanga mwenyi umri wa miaka karibuni miwili ameogotwa akitupwa ndani ya kiwanja kwenyi kata Bujovu mjini Goma.

Kutokana na kiongozi ahusikae na ukingo wa mtoto huko Bujovu , Bwana Maurice NSENGIYUMVA ni viongozi wa tabaka za msinji ndio walipasha habari kuhusu kutupwa kwa mtoto eneo hilo .

Tulijielekeza mahali hapo ili kuogota mtoto na kuarifu serkali kupitia kazi za upelelezi . Baadae kupeleka mtoto kwenyi kituo cha afya ili kuchunguza kama hana maradhi ya ukimwi. Na hapo kumupeleka kwenyi jamaa ya mapokezi kwa muda aeleza Prezidenti ahusikae na ukingo wa mtoto

Huyu anena kuwa ilibidi kuja kweyi ofisi ya mea na baadae kwenyi mtaa wa karisimbi ili atolewe jina na serkali kisheria.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire