Kivu ya kaskazini :Walimu wanaojumwika ndani ya shirika la kutetea haki yao FOSYNAT hawata rudi shule bila suluhu kwa madai yao

Prezidenti wa shirika la kutetea haki ya walimu Kivu ya kaskazini Bahala Shamavu.

Katika mkutano wao majuzi walimu wanaojumwika ndani ya shirika FOSYNAT wamekataa kata kata kurudi shuleni ingawa serkali hatajibu kwa madai yao mapema.

Walinena hayo mbele ya wandishi habari baada ya mkutano mjini Goma mji mkuu wa jimbo la kivu ya kaskazini.

Kutokana na Bwana Bahala Shamavu prezidenti wa shirika FOSYNAT Kivu ya kaskazini, walimu waomba wenzao wapya na wale bado kulipwa wote walipwe mishahara yao na serkali. Pamoja na hayo waomba kuongezewa mishahara, pia wahudumiwe kiafya.

Huyu aongeza kuwa walimu wa shule za msinji na sekondari waomba marupu rupu kuhusu pesa ambazo ni bajeti ya serkali jimboni ,maana humo mwapatikana sehemu yao.

Kuhusu shule za sekondari, walimu wa FOSYNAT kupitia kiongozi wao waomba kuundwe sheria jimboni ili kuanzisha vema mwaka wa shule. Na kwamba sheria yenyewe isipange pesa kwa walimu ambazo ni chini ya zile zilipangwa mwaka iliopita.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire