Goma: Moïse KATUMBI atembelea wahanga wa mripuko wa volkeno

Prezidenti wa Ensemble pour le changement akitembelea wahanga wa moto wa volkeno

Prezidenti wa Muungano wa kisiasa Ensemble pour le changement Moïse KATUMBI TCHAPWE amewasili hii juma tatu mjini Goma ambako alienda kupongeza wahanga wa mripuko wa volkeno waishio ndani ya kempi pa Nyiragongo.

Baada ya kuwasili kunako uwanja wa ndege mjini Goma, alijielekeza haraka kwenyi kempi ya Kahembe ambako wapatikana maelfu ya wahanga wa ajali hiyo ya moto.

Huyu alipeleka chakula ajili ya kujibu kwa hitaji zao, na kunena kuwa raia jimboni Katanga walitoa mcango wa dola mia tatu elfu za marekani ajili ya wahanga. Wakimpokea kwa shangwe na vigelegele. Popote alitembelea raia waliendelea kufwata mlolongo wa gari zilizo msindikiza.

Mbele ya wahanga alisema kukerwa na shida iliyokumba watu hao: « Nilikuja nami ili kuwapongeza kuhusu shida iliyokumba ijapo nilikuwa bado kufika ili moyo wangu ulikuwa n’a haja ya kuja waona mimi ndimi « anena Prezidenti wa ensemble pour le changement Moïse KATUMBI.

Na wakati wa jioni alikutana na wandishi habari ambao alijibu kwa swala kadhaa.

Kuhusu huduma kwa wahanga wa mripuko wa volkeno, alinena kuwa serkali imepiga hatua ya kwanza ila kunabaki mengi ya kufanya. Akiomba yeyote wa moyo mwema kutoa mcango kuhusu watu hawa.

Maswala mengine kuhusu uongozi wa kijeshi Kivu ya kaskazini, kutokuwa mara kwa mara mjini Goma, ujenzi wa ofisi nzuri pya Muungano wao wa kisiasa mjini Goma na kadhalika alijibu bila shaka.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire