Goma : Waziri wa kilimo NZINGA BIRIHANZI aanzisha kazi za ujenzi wa gala kubwa ni katika mradi wa kuinua mlimo Kivu ya kaskazini ( PASA) maarufu

Waziri wa kilimo nchini DRC, pamoja na liwali wa Jimbo la kivu ya kaskazini akianzisha kazi za ujenzi wa gala

« Mungu aksanti , tutaweka gala kubwa kunako eneo lote la Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo ili ya kuchukua mazao ya walimaji wadogo wadogo. Ni furaha kubwa kwangu kuona walimaji wa Goma wanaona kuuza mazao yao ya shamba na kuipeleka ndani ya gala , na hata kwenyi majimbo mengine ya DRC. Ni furaha kwangu nikiwa mzaliwa wa eneo.

Ni matamshi yake waziri wa kilimo nchini DRC wakati wa kuanzisha rasmi kazi za ujenzi wa gala kubwa yenyi kuweza kupokea tani mia tano ya vyakula toka walimaji wadogo jimboni Kivu ya kaskazini. Sherhe ikifanyika mjini Goma.

Walikuweko viongozi wengine kadhaa toka mjini Kinshasa ,pamoja naye liwali wa Jimbo Constant NDIMA akiongoza ujumbe.

Kiongozi wa mradi kimataifa husika na maendeleo ya kilimo Kivu ya kaskazini PASA kwa maarufu Daniel MIHINDO ashukuru serkali ya DRC na wafadhili wake kwa kutekeleza miradi kwa manufaa ya raia wa Kivu ya kaskazini.

 » Mradi PASA Kivu ya kaskazini ambao ni wa serkali ya Kongo unahudumia raia kuhusu usalama ki malisho na kuinua mali ya wakulima wadogo wadogo jimboni Kivu ya kaskazini. Na twaweza fikia lengo hili ingawa walimaji wamehudumiwa kwa mbegu , mboleo na hata dawa za mimea. Pamoja na hayo walimaji wapewe mafunzo kupitia walimu husika na kazi za kilimo anena kiongozi huyu

Huyu asisitiza kuwa gala lenyi kupokea tani mia tano ya chakula litaruhusu walimaji wadogo kukutana na wateja wao wakifaidia kila moja upande wake, akishukuru kwa juhudi za Raisi wa DRC kupitia serkali yake Michel SAMA LUKONDE.

Akishukuru pia kwa juhudi zake Raisi wa DRC, Felii Antoine TSHISEKEDI , liwali wa Jimbo la kivu ya kaskazini Constant NDIMA aahidi kuunga mkono mradi ili ufike ukingoni. Akigusia pia vifaa yaani mbegu kwa wakulima , mboleo, na hata dawa kwa mimea na kadhalika.

Tufahamishe kwamba kazi zitaongozwa naye Injenia Patrick Munembwe wa shirika One Construction DRC kutoka shirika PASA ambayo ni mradi wa serkali ya DRC .

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire