« Ninafurahi sana kwa kuwa tunajenga gala ya kuweka viazi vya kizungu. Matatizo walio nayo walimaji ndani ya mji na wilayani yatakwisha. Tutaanza kwenda nunua vyakula , tunapana pesa, tunaleta vyakula ndani ya gala na kuipeleka kwenyi majimbo mengine na hata nchi za ugenini. »
Hayo ni matamshi yake waziri wa kilimo nchini DRC wakati wa sherehe za kuanzishwa kwa kazi za ujenzi wa gala kubwa la kuweka vyakula mjini Goma hii juma tatu tarehe 4 oktoba 2021. Gala litaweza pokea tani elfu mia tano ya chakula
Walikuweko viongozi kadhaa wa jimbo la kivu ya kaskazini wakiongozwa naye liwali wa jimbo na wengine toka mjini Kinshasa.
Waziri wa kilimo alishukuru Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI kupitia serkali yake waziri mkuu Michel Sama LUKONDE kujiunga kwa manufaa ya raia. Na kumutuma ili kuanzisha kazi za ujenzi wa gala hilo likiongozwa na PASA ambao ni mradi wa serkali ya DRC kwa usapoti wa wafadhili ili kuboresha maisha ya wanainchi .
Akigusia pia swala la uongozi wa kijeshi na kusema kuwa mabadiliko yapo kuhusu kazi hiyo hata kama kuna watu wenyi nia mbaya wasiokubali juhudi zinazofanyika upande wa kijeshi. Aomba raia kuacha mambo ya vita kwa kutekeleza amani ya kudumu
Liwali wa jimbo wa Kivu ya kaskazini Constant NDIMA ameahidi kusindikiza mradi huo ili ufikie lengo. Akionyesha umuhimu wakuhudumia wanavijiji kwa vifaa yaani mbegu, mboleo na hata mafunzo ili wafaulu ndani ya kazi ya kilimo . Hayo yatapelekea wanteja kufika na kununua na faida itaonekana pande mbili kwa walimaji na hata kwa wateja wao.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.