Goma: Rubens MIKINDO aunga mkono juhudi zake liwali wa Jimbo la kivu ya kaskazini kusaka Amani

Waziri wa taifa wa zamani ahusikae na mafuta ya petroli Rubens MIKINDO asema kufurahishwa na hatua yake liwali wa Jimbo la kivu ya kaskazini constant NDIMA kuchukua hatua ya kutekeleza amani na maendeleo wilayani Walikale ambako alifanya ziara juma lililopita.

Rubens MiKINDO anena hayo kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii ijumaa akitokea wilayani Walikale makwao.

Akihojiwa na wandishi habari kuhusu ziara yake , yeye alinena kuwa baada ya kusindikiza liwali alibaki ili kuhamasisha raia kuhusu chama UDPS huko.

Mfanya siasa huyo anena kuunga mkono hatua iliyochukuliwa na liwali pamoja na raia wa Walikale ili kutekeleza maendeleo wilayani humo ambayo imekwama tangu awali.

Waziri Rubens MiKINDO afahamisha pia kusindikiza liwali katika kutafuta suluhu kwa usalama mdogo jimboni hususan wilayani Walikale, kwani siyo tu Walikale tu ndio yakumbwa na hali hiyo.

Waziri wa zamani haunge mkono wale wenyi kusambaza habari za uongo kuwa kuna mganyiko ndani ya chama UDPS mjini Goma.

Chumba cha uhariri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire