Kiongozi wa shule la msinji Amani Byamungu Mudekereza John ahakikisha kuanza kinaganaga mafunzo tangu mwanzoni mwa mwaka ni sasa zaidi ya wiki mbili. Akishukuru wazazi wanaokubali kazi wasifanyazo kwa kuwatumia watoto. Nakuomba wazazi wengine kutobaki nyuma bali watume pia watoto wakingojea matokeo kuhusu kazi zao.
Anena hayo kwa mwana ripota wa la ronde info ijumaa iliyopita mjini Goma.
» Gisi ulivyo jionea binafsi kazi zafanyika bila shaka kwenyi shule Amani. Hakuna vurugu tangu serkali kuanzisha rasmi mwaka wa shule. Tangu tarehe 4 oktoba 2021, twapatikana shuleni hata kama walimu wa shule za serkali wabaki nyumbani. Sisi kama shule la kipekee twapokea watoto afasiria kiongozi.
Kuhusu pedagojia, kiongozi Byamungu Mudekereza aeleza kuwa yote yachunguzwa kwa makini.
» Nilipenda julisha kwamba Shule Amani laheshimu mpango wa kazi toka serkali ya nchi , laheshimu pia saa na yote yaliyomo ndani ya mpango dhidi ya shule la kipusi, msinji na sekondari. » Akiongeza kuwa wazazi wajitahidi kuwatumia watoto bila shaka.
Mpango wa kazi kwa wiki
Kiongozi huyu agusia jisi kazi zafanyika kwa wiki. Kawaida watoto chini ya cshule la msinji wasoma tangu juma tatu hadi ijumaa. Ijapo walimu wao huja ili kutayarisha kazi wiki ifwatayo. Kuhusu Shule la msinji na sekondari , kazi zafanyika tangu juma tatu hadi juma mosi.
Kiongozi asisitiza pia kuhusu saa za kuanza mafunzo na za kukomesha.
» Kwenyi primary school mfano ni saa mbili kamili ndiyo kazi zaanza na kuhitimishwa saa sita dakika arubaini na tano. Na kunako shule la sekondari ni tangu saa moja na nusu hadi saa saba ila siku moja moja saa zaongezeka ili kuelimisha vema watoto « , afasiria kiongozi huyu.
Shule Amani lahusika pia na uchukuzi wa watoto
« Basi nne miongoni moja ndogo na tatu kubwa ili kupeleka watoto nyumbani katika pembe zote mjini Goma » aongeza kiongozi wa shule.
Byamungu Mudekereza John aomba wazazi kutambua gari zenyewe zenyi rangi ya samawi na nyeupe zikitembea popote mjini Goma na kandokando.
Ujumbe kwa wazazi
Kiongozi huyu ashukuru wazazi wote wanaotuma watoto kwenyi shule Amani ili wapate elimu ya kweli.
« Nashukuru wazazi wanaotuma watoto kwenyi shule Amani. Nawahakikishia kuwa watafurahi kwani tunao walimu wenyi ujuzi na ni jambo wanalo lifahamu. Na kwa wengine bado kutuma wafanye haraka na baadae kungojea matokeo bora kulingana na kazi za watoto, » huyu anena.
Kwa mafasirio, Shule Amani lapatikana kwenyi barabara Terminus ULPGL , kunako kiingilio ya hospitali ya wagonjwa wa kichwa , katika kata Kyeshero mtaani Goma Kivu ya kaskazini.
Juvénal MURHULA
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.