Muungano UWEZO AFRIkA INITIATIVE umeandaa juma tatu tarehe 15 oktoba mkutano mkuu uitwao : Maombi kwa roho za marehemu ili kusaka amani« . Hayo yalifanyika mjini Goma katika nyimbo za kuomboleza , ushuhuda, michezo mbali mbali na kadhalika.
Kutokana na kiongozi wa Muungano UWEZO AFRIkA INITIATIVE Douce NAMWEZI sherehe hiyo ni alama ya kukumbuka, kulia na kuombea roho za wote waliopoteza maisha yao katika vita mbali mbali nchini DRC.
Kwake Douce NAMWEZI, ilibidi kufika pa Kaniola jimboni Kivu ya kusini ambako mauaji yalifanyika, kuimba na kufanya michezo kiutamaduni namna ya kupongeza raia wa huko ambao waliishi maafa, ili wawe na matumaini ya amani
Akinena kuwa ni muda wa Jimbo la kivu ya kaskazini ambako vifo vya ripotiwa kila leo, hasa mjini Béni na hata kufikia mjini Kinshasa.
Kiongozi wa Muungano UWEZO AFRIkA INITIATIVE anena kuwa watu wa moyo mwema walijiweka pamoja ili kutafuta namna ya kuhudumia wakongomani walio sumbuka kupitia maafa za vita. Watu hawa walichukuwa hatua ya kujiweka pamoja wakiendesha utetezi kwa kila ngazi ili kutafuta amani nchini.
Tufahamishe kwamba UWEZO AFRIkA INITIATIVE inatumika kwa ushirikiano na Askofu wa Bukavu François Xavier MAROYI , Le prix Nobel pour la paix Denis MUKWEGE, shirika la Uswisi, na wahusika wengine wa mahali wa taifa na wa kimataifa.
Juvénal MURHULA
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.