Waziri ahusikae na vyuo vikuu na yunivasti nchini DRC Muhindo Nzangi Butondo yupo ziarani jimboni Kivu ya kaskazini. Huyu akuja kukomesha mwaka wa shule 2020-2021. Pamoja na hayo kuanzisha mwaka 2021- 2022.
Baada ya kukutana viongozi mbali mbali wa vyuo vikuu na yunivasti jimboni Kivu ya kaskazini, alikutana kwenyi uwanja wa UNIGOM na wanachuo wengi.
Katika hotuba yake waziri Muhindo Nzangi aliahidi kufupisha miaka ya mafunzo kwenyi vyuo vikuu na yunivasti. Pahali pa miaka tano mafunzo yataanza fanyika muda wa miaka tatu , mafunzo yaitwa MLD.
Muhindo Nzangi Butondo aahidi kujihusisha na majengo bora ya vyuo vikuu na yunivasti, na zile zisizo eneza shurti zitavunjwa.
Waziri aongeza kwamba atajihusisha na teknolojia nyipya akitekeleza mawasiliano ndani ya shule hizo. Asema kuwa tayari ameanzisha mradi wa mawasiliano WIFI kwenyi UNIKIN, na baadae Lubumbashi, Goma na kadhalika. Pia uchukuzi kwa shule hizo akitoa basi ambazo aomba wanachuo kutunza vizuri.
Baada ya mcana kati alitembelea vyuo vikuu na yunivasti mjini Goma na kando kando ili kujionea jisi kazi zafanyika. Akiahidi kutembelea vyuo vikuu na yunivasti pa Béni , Butembo na baadae mjini Bukavu.
Juvénal MURHULA
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.