Goma : Kiongozi wa Kamisheni husika na ukingo barabarani Kivu ya kaskazini arudi Goma toka Kinshasa katika ziara ya kazi

Kiongozi wa Kamisheni husika na ukingo barabarani Kivu ya kaskazini

Akihojiwa na wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Bwana Nova Kasimu Saidi anena kuwa amekutana na wenzake wa Kinshasa na Congo ya kati . Hawa walibadili fikra kuhusu ujuzi ndani ya kazi wazifanyazo kila leo. Hiyo ni moja wapo ya ushirika wenyewe kwa wenyewe.

Akiongeza kuwa uhusiano huo utatanda kwa majimbo mengine ya DRC ili kuboresha kazi kwenyi sekta hiyo yenyi kuhusika na ukingo barabarani.

Akijibu kuhusu yale raia wa mji wa Goma watafaidia kuhusu ziara yake , huyu anena kuwa raia watafaidia mengi kuhusu ziara. Akisisitiza kwamba inabidi kwanza abadili fikra na viongozi wengine jimboni na yote ni kwa manufaa ya raia.

Tufahamishe kwamba huyu alipokelewa na viongozi wa CNPR jimboni Kivu ya kaskazini katika hali ya shamra shamra.

Juvénal MURHULA

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire