Kivu ya kaskazini : Nyiragongo: Wakaazi wa Kijiji Rukoko wachukua hatua ya kujihusisha na maendeleo ya kwao

Kiongozi wa Kijiji Rukoko Riphin NDAMBI aomba wakaazi wa Kijiji hicho kutowa mcango kila moja ili kununua nafasi ambayo ni shamba la wafu eneo hilo. Akisisitiza kuunga mkono polisi ili kutekeleza usalama.

Huyu anena hayo baada ya kikao na wakaazi wa kijiji Rukoko hii juma pili tarehe 31 oktoba 2021 pa Nyiragongo.

Kuhusu usalama , yeye aomba wakaazi kutumika bega kwa bega na askari polisi maana wengi mwa wakaazi wanena kuzorota kwa usalama kila leo huko.

Mwakilishi wa polisi kwenyi kikao aahidi usalama kwa raia ingawa wataweza kumuunga mkono.

Waligusia pia swala la moto wa umeme, barabara na kadhalika. Kiongozi wa kijiji Rukoko aahidi kwamba malalamiko yote yatafikishwa kwenyi ngazi za juu ili kutekeleza usalama na maendeleo eneo hilo.

Tufahamishe kwamba wakaazi wamepanga kukutana siku za usoni ili kuweka mkazo kuhusu kununuliwa kwa nafasi ya shamba la wafu.

Juvénal MURHULA

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire