Mwaka wa shule 2020-2021 ulihitimishwa hii juma mosi tarehe 30 oktoba kwenyi Vyuo vikuu na yunivasti eneo lote la Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Mjini Goma yunivasti na vyuo vikuu viliandaa sherehe ili kukomesha mwaka 2020-2021 na kuanza mwaka mpya 2021-2022.
Kunako Chuo kikuu ISC mjini Goma, liwali wa Jimbo la kivu ya kaskazini Constant NDIMA KOGBA ashukuru shule hilo kuhitimisha mwaka ijapo shida chungu télé yaani maradhi ya covid 19 , mripuko wa volkeno na mengineo.
Akiambia wanachuo kwamba jamii yangojea kwao kazi nzuri namna ya kupatia samani cheti walizozipewa
Constant NDIMA ashukuru Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI ambaye ajitahidi kuhusu mafunzo bora ya watoto akisisitiza kuhusu majifunzo kwa bure.
Liwali wa Jimbo ashukuru pia viongozi wa ISC na washirika wake ili kufaulu kwa mwaka huu.
Na kwenyi Chuo kikuu ISIG ni mwanachuo Baraka Bigega wa darasa la nne L2 kwa kimombo ndiye alifaulu na alama nyingi asilimia themanini 80% .
Kiongozi wa shule hilo, ashukuru wanachuo wazazi , viongozi wa nchi , walimu na wafanya kazi wengine kwa mcango wa kila moja ili kufikia lengo.
Kiongozi wa ISIG/ Goma aongeza kuwa shule ISIG Goma lapigania majengo bora, vifaa vizuri vya kazi , uhusiano na yunivasti za taifa na hata zile za kimataifa, kubadili kuhusu ujuzi kati ya wanachuo wa ISIG na wa yunivasti zingine.
Huyu atarajiya shule lake liwe kwenyi mustari wa mbele ulimwenguni.
Tufahamishe kwamba sherhe zingine za kukomesha mwaka wa shule zilifanyika kwenyi yunivasti na vyuo vingine vingi mjini Goma mfano ISTMAC, UNIGOM. ISTA, ISP na kadhalika.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.