Kivu ya kusini : Shirika nyipya la raia latetea kuhusu ujenzi wa barabara mjini Bukavu na kwenyi wilaya

Hali ya barabara zimoja jimboni Kivu ya kusini

Habari toka Shirika hilo Kivu ya kusini zaeleza kuwa barabara nyinyi zapatikana katika hali mbovu kwenyi mitaa mjini Bukavu na kunako wilaya.

Shirika Nyipya la raia latowa mfano wa mtaa wa Kadutu ambako karibu barabara zote zapatikana katika hali ya kutisha. Kuanzia kwenyi Nafasi ya uhuru, Industriel, Kasali. Yesu yesu na penginepo.

Mtaani Bagira, kutokea Nafasi ya uhuru hali yaanza kuwa mbovu tangu shule la Bwindi hadi jumba la mtaa wa Bagira. NDSCi anena kwamba barabara lajaa shimu ndogo ndogo. Pia tangu jumba la mtaa wa Bagira hadi Quartier D upande wa Nyakavogo.

 » Mvula zinaponyesha gari zashindwa kupanda . Katika tu mtaa huo wa Bagira upande wa Kasha, Barabara Bralima, Mushekere hadi Cikera lapatikana katika hali ya hatari. Barabara Busoka, Ciriri ni shida Pia, gari hukwama kila leo wakati wa mvua. Pamoja na hayo barabara Pharmakina, Kahero, Cikera yaomba nayo kukarabatiwa  » duru zaeleza.

Na kuhusu mtaa wa Ibanda , Shirika hili lagusia barabara yenyi kuelekea kunako shule la Ibanda, barabara upande wa avenue Saio na kadhalika.

NDSCI hakusahau barabara ndani ya wilaya, mfano wa barabara nambari mbili Bukavu, Walungu. Barabara Bagira, Kabare kuelekea upande wa hospitali ya Mukongola zote ni katika hali ya hatari.

Barabara Essence Maria Kachelewa hadi vijijini yaani nambari tano na kadhalika.

Shirika Nyipya la raia kupitia prezidenti Wilfried Habamungu lashangaa kuona jimbo la kivu ya kusini peke limeachaliwa kuhusu barabara kulingana na majimbo mengine.

Ndipo laomba serkali jimboni Kivu ya kusini kufanya utetezi kwenyi tabaka za juu ili kujenga barabara hizo , hata ujenzi usiowa kawaida kwa kungojea. Serkali ya Jimbo ifanye iwezekanayo ili kukarabati barabara nyinyi zenyi hali mbovu pahali pa kubaki kimya. Pia kucunguza kazi za madreva barabarani ambao wapandisha bei ya uchukuzi kinyume na sheria hasa mvua zinaponyesha.

Chumba cha uhariri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire