Hali yaendelea kuwa ya wasi wasi mjini Bukavu ingawa milio ya risasi kupunguwa na raia wamoja kutoka nyumbani.
Ndizo habari tunazo kwa sasa kuhusu milio ya risasi iliyosikika tangu usiku wa juma nne saa saba mjini Bukavu.
Shirika la raia mjini Bukavu liliomba raia kubaki kimya nyumbani wakingojea mafasirio ya viongozi wa jimbo kuhusu hali hiyo.
Duru zetu hunena kuwa viongozi hawaja tamka lolote lile tangu hali iliweza badilika mjini Bukavu
Raia huzani kwamba ni kundi lenyi kumiliki silaha kwa jina la wazalendo ao wanamugambo Mai mai na wengineo ndio waliweza kwamisha usalama wakizibiti eneo kadhaa za mji wakipambana na jeshi la taifa FARDC.
Tufahamishe kwamba hakuna matokeo kwa sasa kuhusu hali hiyo ya heka heka.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.